LEARNING HUB

Elewa mwili wako. Kisha jenga hatua unazoweza kuishi nazo.

Masomo haya ni mwanzo wa maktaba ya JENGA MWILI. Tutakuwa tunaongeza articles, videos na resources mpya bila kubadilisha muundo wa website.

01 • CHAKULA

Meal structure kuliko sheria 100

Mpangilio rahisi hukusaidia kujua lini na jinsi ya kula bila kuanza kila siku kutoka sifuri.

Soma muhtasari

Anza na meals zinazoeleweka, protein na mboga, maji na mazingira yanayokusaidia kufanya chaguo bora. Mpango mzuri ni ule unaoweza kuutekeleza mara nyingi.

02 • INSULIN & HOMONI

Homoni kwa lugha ya kawaida

Insulin ni homoni muhimu inayohusika na matumizi na uhifadhi wa nishati. Si adui, na si maelezo ya kila tatizo la uzito.

Soma muhtasari

Ubora wa chakula, kiwango cha activity, usingizi, dawa, mazingira na hali binafsi vinaweza kuathiri jinsi mwili unavyosimamia nishati. Elimu yetu huepuka diagnosis za mtandaoni.

03 • NJAA & APPETITE

Njaa si ukosefu wa nidhamu tu

Usingizi, stress, mazingira, routine na aina ya meals vinaweza kuathiri appetite.

Soma muhtasari

Badala ya kujilaumu, chunguza pattern: ulilala vipi, meal yako ilikuwa na nini, ulikuwa na stress kiasi gani, na mazingira yalikusukuma kufanya chaguo gani.

04 • USINGIZI & STRESS

Maamuzi ya kesho huanza usiku

Usingizi mzuri unaweza kusaidia nishati, appetite na uwezo wa kufanya maamuzi yenye makusudi.

Soma muhtasari

Weka muda wa kutulia, punguza mwanga mkali kabla ya kulala, tengeneza routine inayojirudia na zungumza na daktari ikiwa una tatizo la usingizi linaloendelea.

05 • MOVEMENT

Movement inayoweza kurudiwa

Kutembea na mazoezi yanayolingana na uwezo wako ni bora kuliko mpango mkali unaoishia baada ya siku chache.

Soma muhtasari

Anza mahali ulipo. Ongeza hatua taratibu, linda joints na tafuta ushauri wa mtaalamu ikiwa una maumivu, jeraha au hali ya kiafya.

06 • ACCOUNTABILITY

Elimu bila utekelezaji haijakamilika

Accountability hufanya maendeleo yaonekane, changamoto zijadiliwe na mpango urekebishwe.

Soma muhtasari

Lengo si kukufuatilia kwa hofu. Ni kukusaidia kuona ukweli wa wiki yako, kusherehekea progress na kufanya marekebisho mapema.

VIDEO LESSONS

Unapendelea kujifunza kwa kutazama?

Fungua sehemu yetu ya video au tembelea official YouTube channel ya JENGA MWILI.

Taarifa muhimu: Maudhui haya ni elimu ya jumla. Hayatumiki kufanya diagnosis na hayawezi kuchukua nafasi ya huduma ya daktari au mtaalamu mwingine wa afya.